Mshauri Mkuu wa Chama cha siasa nchini Tanzania cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa chama hicho.
Maalim Seif amechukua fomu hiyo leo Alhamisi Januari 30, 2020 ofisi ndogo ya chama hicho Vuga Mjini Unguja na kukabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Doroth Semu.
Baada ya kupewa fomu, Maalim Seif amesema sababu kuu ya kuwania nafasi hiyo inatokana na uwezo wake pamoja na uzoefu alionao wa kisiasa kwa zaidi ya miaka 25 hivi sasa.
Amesema kupitia uzoefu huo ana amini nafasi ya uenyekiti taifa ataweza kuihudumia kwa lengo la kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Chama hicho, ambacho hivi sasa kinapanga safu zake za uongozi kwa mujibu wa katiba.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment