Kilichoendelea Mahakamani Katika Kesi ya Mume Anayetuhumiwa Kumuua Mkewe kwa Kumchoma Moto

Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mfanyabishara Hamisi Luongo anayetuhumiwa kumuua Mkewe na kumchoma kwa gunia la mkaa, umeutaka upande wa mashtaka kukamilisha uchapishaji wa jarada la kesi hiyo ya mauaji ili shauri liendelee.

Hayo yamebainishwa na upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally baada ya Wakili wa Serikali, Janeth Magoho kuieleza Mahakama ya Kisutu kuwa jarada halisi la shauri hilo lipo Polisi kwenye hatua ya kuchapwa.

“Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini jarada halisi lipo polisi kwenye hatua ya uchapishaji hivyo naiomba Mahakama hii iahirishe kesi hii”- Magoho.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi February,2020 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.


from MPEKUZI

Comments