Kangi Lugola Kuhojiwa na TAKUKURU Kesho

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola anatarajiwa kuhojiwa kesho na Taasisi ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema walianza kukusanya taarifa za awali ambazo zimeshakamilika na wahusika wote wataitwa kesho kuhojiwa.

Rais Dkt John Magufuli alitengua uwaziri wa Lugola kutokana na tuhuma za utiaji saini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya Zimamoto na Uokoaji vyenye thamani ya Euro Mil. 408.2 kutoka kampuni moja ya nje ya nchi.


from MPEKUZI

Comments