Jeshi La Polisi Mkoani Arusha Laua Majambazi Watano

Watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika majibizano na askari polisi mkoani Arusha.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha,Kamanda wa polisi  Jonathan Shanna amesema kuwa,tukio hilo limetokea januari 29 mwaka huu majira ya saa 3:45 asubuhi katika njia panda ya Mateves kata ya Olmot Halmashauri ya Jiji la Arusha.
 
Kamanda Sabas alisema kuwa,tukio hili limetokea baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za siri kuwa majambazi hao walikuwa wamepanga kwenda kufanya tukio la ujambazi katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
 
Alisema kuwa,majambazi hayo walipanga kutumia barabara ya Afrika Mashariki (Bypass) kupitia Olasiti Hadi mzunguko wa kwa mrombo kwa kutumia usafiri wa pikipiki tatu ambazo walikuwa nazo .
 
Amesema kuwa,Mara baada ya polisi kupata taarifa hizo waliweka mtego katika njia panda ya Mateves ambapo ilipofika majira ya saa 3:45 usiku Askari hao waliona pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatokea upande wake Mateves kuelekea barabara mpya ya Afrika Mashariki ,ambapo walisimamishwa na Askari hao lakini badala ya kutii amri majambazi hayo walianza kufyatua risasi.
 
Ameongeza kuwa,baada ya hapo  ndipo kikosi kilianza kujibu mapigo ambapo majibizano hayo yalichukua muda takriban dakika 35 , ambapo majambazi wanne walifariki hapohapo huku jambazi mwingine Mmoja aliyekuwa nyuma aligeuza na pikipiki yake na kukimbia umbali was mita 500 lakini naye alipigwa risasi na kudondoka.
 
“Majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazi hao waliokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki tatu, yalidumu kwa dakika 35 ambapo baada ya kuwaua katika eneo la tukio kulikutwa vitu mbalimbali ikiwamo bunduki aina ya Short Gun Pump Action iliyokuwa na namba 32265-02, Chinese pistol iliyofutwa namba za usajili, bastola moja bandia, risasi na simu tatu,” amesema Kamanda Shanna.
 
Alitaja vitu vingine kuwa ni magazine mbili za Chinese ,Pistol moja ikiwa na risasi 8 na nyingine ikiwa na risasi 1 .maganda 7 ya risasi ya Chinese Pistol,risasi 2 za bunduki aina ya Shortgun,maganda 5 ya risasi ya Shortgun na simu mbili aina ya Tecno na moja aina ya Oking.

Amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa bunduki hiyo aina ya Shortgun pump Action iliibiwa Januari 26 mwaka huu jijini Arusha, saa tisa usiku nyumbani kwa Jackson Msangi baada ya majambazi hao kuvunja nyumba yake iliyopo eneo la Burka ambapo pia waliiba simu ya mke wake Nikira Msangi na wote wawili walipoitwa wametambua mali zao ambazo ziliibwa siku waliyovamiwa.
 
Aidha miili ya marehemu imehifadhiwa ktika hospitality ya mkoa ya Mount meru kwa uchunguzi wa Daktari na utambuzi.


from MPEKUZI

Comments