Wajerumani: Trump ni hatari kubwa kwa amani na usalama wa kimataifa

Uchunguzi mpya wa maoni umeonyesha kuwa, raia wengi wa Ujerumani wanaamini kwamba, Rais Donald Trump wa Marekani ni hatari kubwa zaidi kwa usalama na amani ya dunia.

Ripoti iliyochapishwa na mtandao wa NTV wa Ujerumani imesema kuwa, uchunguzi mpya wa maoni wa taasisi ya YouGov uliofanyika kwa maagizo ya shirika la habari la Ujerumani unaonesha kuwa, Rais wa Marekani Donald Trump anatambuliwa na Wajerumani kuwa ndiyo hatari kubwa zaidi kwa usalama na amani ya dunia.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, asilimia 41 ya Wajerumani wanasema Trump ni hatari kubwa zaidi kwa usalama wa dunia akifuatiwa na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ambaye asilimia 17 wanasema ni hatari kwa usalama wa kimataifa. Asilimia 8 ya Wajerumani wanasema Rais Vladimir Putin ni hatari kwa amani na usalama wa dunia.

Mwaka 2018 pia taasisi ya YouGov ilifanya uchunguzi kama huu wa maoni ambao pia ulionesha kuwa, Wajerumani wengi wanaamini kwamba, Donald Trump ni hatari kwa amani ya kimataifa.

Uchunguzi kama huu wa maoni uliofanyika katika nchi nyingine za Ulaya katika miezi ya hivi karibuni pia umeonesha kuwa, raia wengi wa nchi za bara hilo hawana imani na Rais Donald Trump wa Marekani.


from MPEKUZI

Comments