Viongozi Wa Asasi Za Kiraia Shinyanga Marufuku Kubadilisha Matumizi Ya Fedha Za Wahisani.

SALVATORY NTANDU
Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga yametakiwa  kutobatilisha matumizi ya  fedha wanazopatiwa na wahisani  mbalimbali kutoka nje ya nchi na badala yake wazilekeze katika malengo mahususi ili kuleta tija na mabadiliko chanya katika jamii wanazozihudumia.

Hayo yamebainishwa Disemba 23 mwaka huu na Kaimu mkuu wa kanda ofisi ya Rais, Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora,  Gerald Mwaitebele, wakati akitoa mafunzo kwa viongozi wa mashiriaka na asasi zisikuwa za kiserikali mbalimbali kuhusiana na sheria ya maadili ya viongozi wa Umma yalifanyika mjini Shinyanga.

“Wapo baadhi ya viongozi wa mashirika na asasi hizi hubatilisha matumizi ya fedha wanazopatiwa na wahisani hususani fedha za kulelea watoto yatima wazee,na makundi mengine katika jamii yasiyo jiweza lakini wapo watumishi wa umma waliokasimishwa majukumu ya kuzisimamia tutahakikisha hawajihusishi na rushwa”alisema Mwaitebele.

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma inakataza viongozi wa asasi hizi kujinufaishwa wenye kuwa kutumia mamlaka yao vibaya ikiwa ni pamoja kutumia fedha za wahisani katika shughuli zao binafsi  jambo ambalo litanaweza kuwakatisha tama wafadhili wao na kuipa sifa mbaya kuhusiana na asasi na mashirika haya.

Awali akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, Mhandisi Maligisa Doto aliwataka viongozi wa asasi hizo kufanya kazi kwa weledi,uazalendo na Uadilifu  katika utendaji kazi zao ili kuisaidia serikali katika ujenzi wa jamii bora .

“Kila kiongozi wa asasi na mashirika yasiyo ya kiserikali anawajibu wa kuhakikisha ana timiza malengo mahususi kwa kuzingatia katiba zao za undeshaji wao ili kuepuka migongano ya maslahi baina yao na jamii wanayoihudumia”alisema Doto.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wa asasi hizo,Mericiana  Stanley katibu mkuu wa taasisi ya Young Women Christian Asociasion (YWCA) na   Joseph Mpagala mkurugezi wa Asasi ya (COWOSE) za mkoani Shinyanga walisema wameipongeza tume ya maadili kwa kutoa mafunzo hayo kwani yamesaidia kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji kazi.

Wamesema endapo viongozi wa umma ambao wamepewa mamla ya kuzisiamia asasi na mashirika hayo kwa weledi vitendo vya rushwa na ubatilishwaji wa fedha za wahisani hautajitokeza pindi wanapopata misaada mbalimbali kutoka kwa wahisani wao kwaajili ya kuihudumia jamii.

“Momonyoko wa maadili katika asasi na mashirika hayo unachangiwa na baadhi ya viongozi wasiokuwa waadilifu tunaiomba serikali kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika mashirika haya pindi inapoona kuna viashiria vya ubadhirifu wa fedha za wahisani au kubatilishwa kwa matumizi bila ya kuzingatia malengo mahususi” alisema Mpangala.

Zaidi  ya asasi na mashirika ya kiraia 30 yamepatiwa mafunzo hayo kuhusiana na sheria ya maadili ya viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 na tume ya maadili kanda ya Magharibi (Tabora).

Mwisho.


from MPEKUZI

Comments