Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha inawekeza katika mistu yao ili kuwa na vyanzo endelevu vya ukusanyaji mapato badala ya kusubiri watu wakosee ndipo wakusanye mapato.
Alisema hatua ya kutegemea kukusanya mapato yanatokana na adhabu kwa waharifu na wanakamatwa na mkaa katika vizuizi hakuwezi kuwafanya kuwa na mapato endelevu.
Kanyasu alitoa kauli hiyo leo Mkoani Tabora wakati akizungumza na wafanyakazi walio chini ya Wizara ya wa Maliasili na Utalii kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa TFS.
Alisema wakati umefika kwa TFS kuwekeza katika msitu yake kwa upandaji wa miti na ufugaji wa nyuki ili kuwawezesha kuwa na vyanzo vya mapato badala ya kusubiri watu wafanye makosa ndio wapate mapato kupitia adhabu wanapatia.
Kanyasu aliongeza kuwa ipo siku watu wanaoharibu mistu watastarabika na kuacha makosa kama vile kukata miti na kuacha kuchoma mkaa bila vibali na hivyo kujikuta hawana vyanzo vya mapato.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa Mkoa wa Tabora kuharakisha mchakato wa kuikabidhi uendeshaji wa bustani ya wanyama pori(zoo) iliyopo Manispaa ya Tabora kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ili iweze kuiendesha kwa faida na hivyo kusaidia katika kuingizia Serikali mapato.
Alisema uboreshaji wa bustani hiyo ni muhimu sana kwa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuwaongezea kuongeza idadi ya watalii na kipato cha Mkoa huo na wakazi wake.
Kanyasu alisema badala ya watalii kwenda moja kwa moja katika vivutio vingine wanaweza kuaniza kwa kutembelea bustani hiyo na hivyo watu wenye Hoteli, Mkoa na wenyeji kujipata kipato kupitia tozo mbalimbali wanazolipa wageni.
Aidha alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikilipa Maaskari wanaolinda bustani hiyo wakati bado haijatumika ipasavyo kuiingizia Serikali mapato na kuongeza kuwa kama Mkoa unaona eneo hilo litumike kwa shughuli nyingine wawaeleza ili wanyama waliomo warudishwe porini na walinzi wapelekwe maeneo mengine yenye upungufu watumishi wa kada hiyo.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema suala hilo tayari Kamati inaendelea kulifanyia kazi na ndani ya siku chache watalipatia ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment