Mama Mzazi wa Erick Kabendera Afariki Dunia

Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki Dunia leo Jumanne Dec 31, 2019 katika Hospitali ya Amana Da es Salaam  alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Bi. Verdiana alionekana hadharani mara ya mwisho  Disemba 13 Mwaka huu akiomba mwanae aachiwe huru kwakuwa anamtegemea kwa matibabu.

Erick ambaye kwa sasa yuko rumande katika gereza la Segerea, Dar es Salaam, alikamatwa Julai 2019 kwa makosa ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kushiriki katika genge la uhalifu.


from MPEKUZI

Comments