Christ Mass Yaondoka Na Watu Wawili Kagera

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,kagera. 
Watu wawili wamepoteza maisha Mkoani Kagera katika matukio tofauti tofauti katika kipindi cha kusherekea siku kuu ya Noeli.  

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera ACP Revocatus Malimi  wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani  humo ambaye ameeleza kuwa matukio hayo yametokea ngara na Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. 

Katika tukio la kwanza Kamanda Malimi amesema kuwa ni la mauji katika wilaya ya Ngara, ambapo marehemu JOVAN JAPHET (36) mkulima na mkazi wa kitongoji cha Kumzenga, kijiji Nakatunga –Ngara alikutwa tarehe 25/12/2019 saa 07:30 ameuawa na  mtu/watu ambao hawajatambulika. 

Kamanda Malimi amesema kuwa  mwili wa marehemu ulikutwa kandokando ya njia baada ya kutoweka kwake kuanzia  tarehe 24/12/2019 saa 12:00 na alikuwa ameanzisha tabia ya kuondoka kwake kunywa pombe bila kuaga kwa mke wake  na kutorudi kwa siku mbili au zaidi. 

Kamanda Malimi amesema kuwa tayari mtuhumiwa wa tukio hilo amebainika na kukamatwa anayefahamika kwa majina ya JEREMIAH  GWASA(26) na sababu ya kuhusishwa kwake zimetokana na kusikika nyumbani kwao mbele ya mama yake akieleza kuwa ndiye aliyefanya tukio hilo kutokana kuchoka kudhurumiwa mali zake na marehemu na taharifa hiyo kufikishwa  Polisi kupitia viongozi wa serikali ya kijiji ambao walipewa taarifa  na mama wa mtuhumiwa baada ya kuchukizwa na kitendo hicho. 

Katika tukio lingine  ni ajali ya mtembea kwa miguu kugongana  na gari/pikipiki na kusababisha kifo. 

Tukio hilo lilitokea tarehe 26/12/2019 majira ya saa 20:00 usiku katika barabara ya Kashozi mtu mmoja mtembea kwa miguu ambaye ametambulika kwa majina ya PAULINE PAULO KARUGILA (55) mkulima na mlinzi wa kampuni ya TTCL na mkazi wa mtaa wa Bugombe Manispaa ya Bukoba. 

Kamanda Malimi amesema kuwa tukio hilo lilitokea wakati akienda kazini aligongwa na chombo  cha moto kati ya gari au pikipiki na chombo hicho kukimbia  nay eye kupoteza maisha hapohapo na kuongeza kuwa juhudi za kukitafuta chombo hicho zinaendelea.


from MPEKUZI

Comments