Bomu lililotegwa ndani ya gari lawaua watu zaidi ya 40 Mogadishu, Somalia

Bomu la kutegwa ndani ya gari limelipuka leo asubuhi katika kituo kimoja cha ukaguzi wa usalama chenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, na kuwauwa karibu watu 76. 


Mkuu wa hospitali ya Medina Mohamed Yusuf amethibitisha idadi hiyo akisema watu wengine 70 wamerujiwa. 

Awali, msemaji wa serikali Ismail Mukhtar alisema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu zaidi ya watu 60 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali. 

Tukio hilo Limekuwa mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kutokea katika siku za karibuni mjini Mogadishu. 

Kapteni Mohamed Hussein amesema mlipuko huo ulikilenga kituo cha kukusanya kodi wakati wa pilikapilika za asubuhi wakati wakazi wakirejea kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa juma. 

Hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu aliyehusika na shambulizi hilo. 

Kundi la itikadi kali la Al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda aghalabu hufanya mashambulizi ya aina hiyo. 
 
Tangu mwaka 2007 kundi la kigaidi la Al-Shabab limekuwa likifanya juu chini kuipindua serikali kuu ya Somalia.

Mwaka 2011, Al Shabab lilifurushwa kutoka mji mkuu Mogadishu kwa ushirikiano wa jeshi la Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika vilivyotumwa nchini humo AMISOM; hata hivyo hadi sasa kundi hilo la kigaidi lingali linashikilia baadhi ya  maeneo ya vijijini nchini humo

Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa kundi la al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.


from MPEKUZI

Comments