Waziri Jenista Mhagama Atangaza Punguzo La Bei Ununuzi Wa Nyumba Za PSSF Za Buyuni-chanika Jijini Dar Es Salaam
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ametangaza punguzo la bei kwa karibu asilimia 50 kwa atakayehitaji kununua nyumba zilizo katika mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) huko Buyuni-Chanika jijini Dar es Salaam.
Mheshmiwa Waziri ametangaza uamuzi huo wa Serikali wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kutembelea vitegauchumi vinavyomilikiwa na Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Novemba 26, 2019 katika eneo la Mradi ambapo nyumba zilizoingia kwenye punguzo hilo ziko 480.
Akitoa mchanganua wa bei mpya Mhe. Waziri alisema, nyumba yenye vyumba viwili vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi milioni 66.80, sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 36.58, nyumba ya vyumba vitatu vya kawaida awali iliuzwa kwa shilingi Milioni 67.260 na sasa itauzwa kwa shilingi Milioni 41.30.
Nyumba yanye vyumba viwili vya kawaida na Master Bedroom ilikuwa inauzwa shilingi Milioni 74.340 na sasa itauzwa Shilingi Milioni 46.20, aidha nyumba yenye vyumba vitatu na Master Bedroom iliyokuwa ikiuzwa shilingi Milioni 83.780 na sasa itauzwa kwa shilinhgi Milioni 61.360.
“Naielekeza Bodi na Menejimenti kuanzia leo (jana Novemba 26, 2019) ninapotoa tamko hili, nyumba hizo zote 204 ambazo hazijapata wanunuzi kabisa na zile 276 ambazo malipo yake yalikuwa bado hayajakamilika ambazo wafanyakazi walikuwa hawawezi kulipa hizo bei za mwanzo, nyumba hizo zote ziingie katika bei niliyotamka leo kwa niaba ya Serikali.” Alisisitiza na kuongeza……
“Baada ya kuona ununuzi wa nyumba hizo si wa kuridhisha, Menejimenti ya Mfuko imenifahamisha juu ya juhudi mbalimbali zilizofanywa kwa maelekezo ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko, na hatua hizi zililenga kupata njia bora ya kuuza nyumba hizi, kwani lengo kuu lilikuwa ni kujenga na kuuza nyumba kwa watumishi na watanzania kwa ujumla na sio kukaa nazo kama sehemu ya uwekezaji wa Mfuko.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Mheshimiwa Waziri alisema uamuzi huo wa serikali unatokana na ripoti ya Mthamini Mkuu wa Serikali baada ya kukamilisha tathmini na thamani halisi ya nyumba hizo kwa sasa.
"Nilipata taarifa kuwa katika mradi huu walikuwepo madalali kuanzia sasa hakuna haja ya kuwa na madalali kwani Mlango uko wazi kwa watu binafsi watakaohitaji kununua nyumba hizi kwani na wao ni watanzania wenzetu.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment