Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ametoa onyo kali kwa makampuni ya ujenzi mkoani humo kutumia magari ya mizigo kinyume na taratibu, kutokana na kuona gari maalumu la kubebea maji likiwa limepakia wafanyakazi wanaofikia 30 wa kampuni ya CRSG inayojenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Njombe –Moronga kwenda Makete wakiwa wamepakiwa juu ya roli la kubebea maji (Boza).
Akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa km 53.9, Mheshimiwa Ole Sendeka ameyataka makampuni yanayotekeleza mradi wa kitaifa wa ujenzi wa barabara za lami na kiwango cha zege ndani ya mkoa wa Njombe kuhakikisha wanatumia gari maalum la kubeba wafanyakazi wao na si kuwapakia kwenye magari yasiyoruhusiwa kubeba abiria ili kuepusha ajari, huku madereva wakitakiwa kutii sheria za usalama barabarani..
“Ni kwanini mkae juu ya boza,kwa hiyo kila siku mnabebana hivi? Kuanzia leo biashara ya kuwapakia hawa wanaokwenda kutengeneza mitaro juu ya boza ife,muiteni huyo meneja wenu mchina na msaidizi wake na HR wenu mripoti ofisini kwangu’anasema Ole Sendeka
Hata hivyo dereva wa gari la kampuni ya CRSG ambaye alinaswa akiwa amevunja sheria za usalama barabarani kwa kupakia wafanyakazi juu ya roli la kubeba maji kinyume na sheria alipohojiwa sababu za kufanya hivyo alisema kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria lakini wamekuwa wakifanya kutokana na mazingira yao ya kazi yalivyo
Kufuatia hali hiyo, kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa alimwagiza mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani mkoa wa Njombe (RTO) kuchukua hatua mara moja.
“Mtakufa ninyi hiki mnachofanya ni hatari na nimeshapiga simu kwa RTO”anasema Hamis issa
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment