Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameagiza mawakala wa mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD) mkoani humo, kukamatwa na kuwekwa ndani kutokana na kutohudhuria mkutano wa wafanyabiashara soko la Sido, jijini Mbeya leo Novemba 30, 2019.
Chalamila ametoa agizo hilo leo Jumamosi katika mkutano wake na wafanyabiashara wa soko hilo kwa ajili ya kusikiliza kero zao.
"RPC watafute leo Jumamosi wapumzike mahali tutakutana nao Jumatatu, haiwezekani huu ni upuuzi tunawahitaji wao hawapo hata sisi tumeacha usingizi," amesema.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Mbeya (TRA), Jiji la Mbeya lina mawakala wanne kwa sasa ambao walitakiwa kuhudhuria mkutano huo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment