Tanzania yaitaka dunia kuiondolea vikwazo vya kuichumi Zimbabwe bila masharti

Na Mwandishi wetu,
Tanzania imelaani vikali vikwazo ilivyowekewa nchi ya Zimbabwe na kuitaka dunia kuiondolea nchi hiyo vikwazo hivyo bila masharti kwani haviaathiri tu Zimbabwe bali huathiri pia nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
 
Kauli ya kulaani vikwazo hivyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati alipokuwa akiwasilisha mada katika kongamano maalum kuhusu "vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu wa Zimbabwe" leo Jijini Dar es Salaam.
 
Prof. Kabudi alisema kuwa kitendo cha dunia kuiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe, hakuiathiri tu Zimbabwe bali hata nchi wanachama wa SADC. 

"Tulikubaliana katika mkutano wetu wa mwezi Augosti kuwa leo tarehe 25/10/2019 kuiambia dunia kuiondolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi ilivyoviwekea bila masharti..…leo siyo siku ya kuomba wala kukumbushana bali leo ni siku ya kuiambia dunia rasmi iiondolea Zimbabwe vikwazo vya kuichumi" Alisema Prof. Kabudi
 
Waziri Kabudi aliongeza kuwa "vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe ni batili na kama Marekani na Umoja wa Ulaya wana hoja ya msingi wapeleke azimio katika baraza kuu la umoja wa mataifa na ndiyo maana katika mkutano wa SADC tuliazimia kulaani vikali Zimbabwe kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kuitaka dunia kuiondelea Zimbabwe vikwazo hivyo bila masharti,".
 
Pia tunasahau sababu ya msingi iliyoifikisha Zimbabwe ktk maamuzi iliyoyachukua, maamuzi hayo kiini chake kikubwa na suala la ardhi ambapo suala la ardhi ni miongozni mwa masuala ambaya hadi Zimbabwe inapata uhuru lilikuwa halijapatiwa ufunguzi. 
 
Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, mzizi wa mambo yote haya ni sheria ya kibaguzi iliyopitishwa na waingereza kwa kusingizia kuwa wameipa Zimbabwe utawala wa ndani mwaka 1923 lakini wao walibaki na mamlaka yote juu ya ardhi. Sheria ile ilikuwa ya kibaguzi kwani ilichukua zaidi ya nusu ya ardhi yote ya Zimbabwe.
 
"Ni wajibu wetu sisi kama Tanzania kuendelea kusimama na Zimbabwe katika kuhakikisha kuwa ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa Zimbabwe inaondolewa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa" Alisema Waziri Kabudi na kuongeza kuwa vikwazo hivyo haviiathiri tu Zimbabwe kiuchumi bala hata nchi wanachama wa SADC wanaathirika hivyo tunaitaka dunia kuindolea Zimbabwe vikwazo hivyo.
 
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia na Wazee, Prof. Jingu alisema kuwa diplomasia ya uchumi imeiwezesha Tanzania kuingia katika uwekezaji, kusaini mkataba, msaada au masoko hivyo tunapaswa kuhakikisha kuwa masuala ya kiuchumi yanapewa uzito wa hali ya juu.
 
"Vita ya kiuchumi imekuwa na athari mbalimbali kwa wananchi kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa ujumla….vita hii ya Zimbabwe kuwekewa vita ya kiuchumi imeleta athari nyingi baadhi ni kukusekana kwa maji safi na salama, kukosekana kwa nishati ya uhakika na ongezeko la mfumuko wa bei ambao umeathiri si tu Zimbabwe, bali hata nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). 
 
Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe vimesababisha anguko kubwa na adha kwa wanachi masikini tena wasio na hatia hivyo ni vyema Afrika itambue kuwa vikwazo hivi vinaweza kutumika kama fursa ya kukuza biashara na uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika. 
 
"Ni muhimu nchi zetu za Afrika zifanye uchambuzi mapema ili kubaini maeneo ambayo ya kimkakati ambayo ni dhaifu na yanaweza kuwekewa vikwazo, na moja ya eneo hilo ni umiliki wa hisa katika makampuni hasa yale makubwa ya kimkakati ili tuweze kuchukua hatua stahiki za kujihami kwa kushirikisha sekta binafsi," Alisema Dkt. Mpango
 
Aliongeza kuwa, vikwazo dhidi ya Zimbawe vimewekwa kimabavu kwani havikufuata taratibu, hivyo ni wajibu wetu sisi kama nchi za SADC kusimama na Zimbabwe kuhakikisha kwamba Wazimbabwe wanarudishiwa ardhi yao na kuondolewa vikwazo vya uchumi.
 
Awali, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye alisema kuwa Zimbabwe inakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi kutokana na maazimio yaliyochukuliwa na nchi za Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya mwaka 2001. 
 
"Vikwazo hivi vimeathiri sana uwezo wa Serikali ya Zimbabwe kiuchumi hususani fursa za mikopo, kupata nafuu ya madeni, na zaidi kupata uwezo wa kutoa huduma kwa jamiii. Zimbabwe inapita katika kipindi kigumu cha msukosuko wa kiuchumi uliogubikwa na mfumuko wa bei, upungufu mkubwa wa bidhaa, chakula na huduma muhimu katika jamii" Alisema Prof. Anangisye
 
Kwa mujibu wa Prof. Anangisye vikwazo vya kiuchumi vipo katika makundi ambayo ni vikwazo vya biashara ambavyo vinalenga mauzo ya nje na manunuzi ya bidhaa za nchi kama ambavyo vilivyowahi kuwekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vikwazo vya kifedha ambavyo vinalenga sekta, taasisi na mfumo mzima wa kifedha ikiwemo misaada, mikopo na mfumo mzima wa fedha za kigeni, na vikwazo vyenye malengo maalum yaani " Targerted Sanctions".
 
Kongamano hilo lilihudhuriwa na vongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali, vyma vya siasa na ujumbe wa balozi za nchi mbalimbali hapa nchini. 
 
Katika kongamano hili, Serikali ya Chini Ikongozwa na Balozi wake nchini Tanzania, Balozi Wang Ke alisema kuwa serikali ya China inasimama pamoja na nchi za SADC katika kuhakikisha kuwa Zimbabwe inaondolewa vikwazo vya kiuchumi.
Mwisho….




from MPEKUZI

Comments