Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema mikoa ya Kanda ya Ziwa itakuwa na mvua nyingi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA, mikoa itakayokumbwa na mvua hizo ni Geita, Kagera, Mara na Magharibi mwa Simiyu.
Aidha, kiwango cha athari kinachoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
Wiki kadhaa zilizopita TMA ilitoa tahadhari ya uwapo wa mvua kwenye mikoa mbalimbali nchini ambayo itaanza Novemba hadi Aprili mwakani.
Aidha, siku chache baadaye Mamlaka hiyo ilitoa utabiri wa mvua kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.
Tangu kuanza kwa mvua hizo, watu 25 wamepoteza maisha katika mikoa ya Morogoro na Tanga, huku madaraja manne yakisombwa na maji na kukatika kwa mawasiliano kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment