Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi Alazwa Tena Hospitali Wiki Mbili Baada Ya Kutoka

Rais  wa Zamani wa Kenya, Arap Moi  amelazwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya Nairobi na madaktari wanasema ni kutokana na maumivu ya kifua na shida katika kupumua

Wiki mbili zilizopita, aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo alipokuwa amelazwa huku Katibu wa Chama cha KANU, Nick Salat akisema Moi alienda kwa uchunguzi wa kawaida wa kiafya

Nick Salat amesema, "Alikuwa hospitalini hapo siku kadhaa nyuma na amerudi tu kwa ombi la madaktari wake. Yeye ni mzee na uchunguzi wa mara kwa mara kwa watu wa rika lake ni kawaida tu."

Mwaka jana, Moi aliondoka kwenda Tel Aviv, Israeli kwa uchunguzi wa matibabu akisindikizwa na mwanawe Gideon na Daktari wake, Dkt. David Silverstein


from MPEKUZI

Comments