Nyavu Haramu Zenye Thamani ya Shilingi Bilioni 8 Zatekeketezwa Kwa Moto Kagera

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera
Zana haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 zilizokamatwa kwenye doria mbalimbali za kukabiliana na uvuvi haramu ziwa Vitoria zimeteketezwa moto mkoani Kagera.
 
Hayo yamebainishwa wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo na Kaimu Afsa Mfawidhi Wa Kitengo Cha Udhibiti Wa Rasilimali Za uvuvi Bw Gabriel Magene na kuongeza kwamba zimekamatwa  kutokana na matokeo ya kazi ambayo zimefanyika kuanzia mwaka huu wa 2019 kuanzia mwezi January. 
 
Bwana Magene amesema kwamba nyavu hizo zina thamani ya shilingi bilioni 8.7 na kuongeza kuwa zimeteketezwa kutokana na mahakama kudhibithisha kuwa ni nyavu haramu na imetoa kibali ziweze kuteketezwa kwa mujibu wa sheria.
 
Amesema kuwa nyavu ambazo zimeteketezwa ni pamoja na nyavu 196 za kokoro za kuvua sangara,nyavu zenye macho madogo chini ya inchi sita 19,620, nyavu 40 za dagaa zenye macho madogo, nyavu za double zenye macho 26 ni 12,000 pamoja na nyavu za monofilament 1,880.
 
Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Marco Elisha Gaguty amewataka wavuvi kuacha kutumia nyavu hizo ambazo aziruhusiwi kisheria na ikibainika wanafanya hivyo sheria itachukua mkondo wake.



from MPEKUZI

Comments