Hukumu ya Jamal Malinzi na wenzake watatu Kutolewa Mwezi Ujao

Hatima ya Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu kurudi uraiani au la itajulikana Novemba 7,mwaka huu watakaposomewa hukumu.

Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335.

Uamuzi huo ulisomwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, baada ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde aliyesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru.

Hakimu alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa pande zote mbili, mahakama yake itatoa hukumu mwezi ujao.

Wakili wa Serikali Ester Martin alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kupanga tarehe ya hukumu na kwamba upande wa Jamhuri uko tayari.

Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itasomwa hukumu tarehe iliyopangwa na kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu.



from MPEKUZI

Comments