Wadau mbalimbali wanaoshiriki Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini jana Septemba 27, 2019, wametembelea Mgodi wa Dhahabu wa GGM unaomilikiwa na Kampuni ya Anglo Gold Ashanti.
Ziara hiyo imelenga katika kujifunza kuhusu namna shughuli za uchimbaji na uzalishaji wa Madini ya Dhahabu unavyofanyika mgodini hapo huku lengo kuu likiwa kuona teknolojia mbalimbali zinazotumika katika uchimbaji wa madini.
Aidha, mbali na kujifunza kuhusu uzalishaji na uchimbaji, wadau hao wameelimishwa kuhusu masuala mazima kuhusu namna mgodi huo unavyoshughulikia masuala ya mazingira, usalama na afya mgodini.
Akizungumzia masuala ya jamii, Afisa anayehusika na Masuala ya Mahusiano na Jamii mgodini hapo Musa Shunasu, ameeleza mgodi huo umekuwa ukitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo, kufadhili miradi mbalimbali, pia kwa kushirikiana na Wizara ya Madini umeanzishwa mgodi wa mfano wa Lwamgasa unaolenga katika kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.
Aidha, mgodi huo umesaidia jamii katika masuala mengine mbalimbali yakwemo ya elimu na afya
Akijibu hoja kuhusu madai mbalimbali ya wananchi kuhusu masuala ya fidia amesema kwamba mwananchi yoyote katika eneo linazunguka mgodi huo ama aliye mbali ya eneo hilo anaruhusiwa kuwasilisha malalamiko yake kwa mgodi.
Kwa mujibu wa Shunasu, kampuni hiyo ina zaidi ya migodi 16 maeneo mbalimbali duniani, huku hapa nchini ulianza shughuli za uzalishaji mwaka 2000.
Amesema Dira ya kampuni hiyo ni kuchimba dhahabu kuwa kampuni inayoongoza kwa uchimbaji, usalama, mazingira na jamii.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment