Waasi wa Yemen Wanaoungwa Mkono Na Iran Wadai Kufanya Mashambulizi Makubwa Saud Arabia na Kuwateka Mamia ya Wanajeshi na Silaha
Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wametangaza jana kuwa wamefanya oparesheni kubwa dhidi ya muungano wa majeshi unaoongozwa na Saud Arabia nchini Yemen na kuwateka mamia ya wanajeshi wa saudi Arabia na waitifaki wake pamoja na kuteka magari mengi ya kivita yanayomilikiwa na Saud Arabia, kusini-magharibi mwa jimbo la Najran.
Hayo yameelezwa na Msemaji wa jeshi la ulinzi la Yemen,Brigedia Jenerali Yahya Saree ambapo pia amesema kuwa katika mapambano hayo, brigedi tatu za kijeshi za Saudi Arabia zimesambaratishwa
Kwenye ripoti iliyotangazwa na shirika la habari linaloegemea upande wa waasi hao al-Masirah, Yahia Sarie amesema kuwa walikamata pia idadi kubwa ya silaha, huku akiongeza kuwa hiyo ndiyo operesheni kubwa zaidi tangu muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoanza kuingilia masuala ya nchi hiyo.
Hakujakuwa na taarifa yoyote kutoka upande wa Saudi Arabia kuthibitisha au kukanusha madai madai hayo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment