Licha ya vikwazo vya Marekani, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema ataendelea kununua gesi na mafuta ya Iran.
Rais Erdogan amesema kupitia kituo cha televisheni cha Uturuki NTV, kwamba Uturuki haihofiii kuadhibiwa na Marekani.
Nchi yake anasema haiwezi kujikosesha mafuta na gesi kutoka Iran. Rais Erdogan anasisitiza ataimarisha ushirikiano wa kiuchumi pamoja na Jamhuri ya Kiislam ya Iran katika sekta nyengine pia.
Lengo anasema ni kuzidisha mara nne biashara iliyopo kati ya nchi hizo mbili.
Rais Donald Trump wa Marekani ameiwekea Iran vikwazo vikali ili kuilazimisha ifikie makubaliano makali zaidi dhidi ya mradi wake wa nuklea.
-DW
Rais Donald Trump wa Marekani ameiwekea Iran vikwazo vikali ili kuilazimisha ifikie makubaliano makali zaidi dhidi ya mradi wake wa nuklea.
-DW
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment