Marekani kupeleka wanajeshi 200 na mifumo ya ulinzi eneo la Ghuba

Mvutano kati ya Marekani na Iran huenda ukaongezeka baada ya Washington kutangaza kuwa inatuma vikosi zaidi vya kijeshi katika eneo la ghuba huku Tehran ikiitaka Saudi Arabia ithibitishe madai kuwa Iran iliishambulia miundombinu ya mafuta ya nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema jana kuwa inapeleka wanajeshi 200 pamoja na mifumo ya kujilinda dhidi ya makombora ili kuimarisha ulinzi wa Saudi Arabia.

Uamuzi huo wa Marekani ambao unajumisha pia kupelekwa kwa rada nne za kijeshi unafuatia mashambulizi ya Septemba 14 kwenye miundombinu ya kuzalisha mafuta nchini Saudi Arabia.

Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Saudi Arabia kila moja  zimeilaumu Iran kuhusika na mashumbulizi hayo. 

Iran kwa upande wake imekanusha madai ya nchi hizo na jana Alhamisi rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani ametaka utolewe ushahidi kuthibitisha kuwa Tehran ilikuwa nyuma ya hujuma hizo.


from MPEKUZI

Comments