Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema serikali imefuta kodi kero 54 kwa wafanyabiashara pamoja na kupunguza mamlaka za kutoa leseni za biashara .
Bashungwa ameyasema hayo mjini Makambako mkoani Njombe wakati akizungumza na wafanyabiashara kutoka mikoa zaidi ya 7 nchini waliokutana mjini hapo kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya biashara na kuja na maazimio ya kuiomba serikali kupunguza utitili wa kodi,tozo na leseni kwa wafanyabiashara ili kunusuru sekta hiyo ambayo imetajwa kuwa katika hali mbaya kimaendeleo kwa sasa.
“Kuna kodi 54 zimeishaondolewa na ili nisiseme tu 54 mheshimiwa mwenyekiti wenu nimeisha mkabidhi hizo kodi kero 5”alisema Bashungwa
Awali wakizungumzia changamoto hizo wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka mikoa ya Tanga, Dar es salaamu,Mbeya,Songwe, Ruvuma, Iringa,Njombe na Katavi wamesema hali ya biashara nchini imezidi kuwa ngumu kwasababu kumekuwa na mrundikano wa tozo na ushuru kutoka mamlaka mbalimbali ikiwemo TRA,Halmashauri na nyinginezo hatua ambayo inawafanya watu wengi kufunga biashara zao.
Amani Mahellah,Sifael Msigala na Ismail Masoud ni baadhi ya wawakilishi walitoa maoni yao katika mkutano huo mkubwa wa wafanyabiashara nchini ambapo wamemuomba waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa kuhakikisha anakutana na wizara zote zinazomgusa mfanyabiashara katika majukumu yake ili kuzitafutia ufumbuzi changomoto hizo kwa ustawi wa sekta ya biashara na taifa kwa ujumla.
“Hizi taasisi zinazokusanya kodi za serikali zikutane kwa pamoja na wafanyabiashara ili kila mtu ajue kwa mfanya biashara yule anachukua shilingi ngapi”alisema Amani Mahellah mmoja wa wafanyabiashara
Akifafanua kiini cha kusuasua kwa sekta ya biashara nchini katibu mkuu wa jumuiya ya wafanyabiashara JWT Abdallah Mwinyi amesema kuwepo kwa urasimu mkubwa bandarini kunawafanya kutengeneza mianya ya rushwa huku kamishna wa TRA nchini Edwin Mhede akimtaka kila mfanyabiashara kuviripoti vitendo vyote vya rushwa kwani vinaikosesha nchini Mapato.
“Forodha aangaliwe kwa makini nap engine sheria zibadilishwe kwenye udhaminishaji na uondoshaji mizigo bandalini” alisema Abdallah Mwinyi
Katika mkutano huo wizara nne zenye mahusiano ya karibu na wafanyabiashara zimealikwa ikiwemo ya viwanda na biashara ,tamisemi, fedha na uwekezaji.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment