Uturuki yapanga kununua ndege ya kivita iliyotengenezwa Urusi chapa SU-57

Viongozi wa Urusi wanazungumza na wenzao wa Uturuki kuhusu uwezekano wa kuiuzia Ankara ambayo ni mwanachama wa jumuia ya kujihami ya NATO ndege za kivita chapa Su-57. Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Urusi amesema.

Rais Recep Tayyip Erdogan ameonyeshwa ndege hiyo ya ufundi wa kimambo alipohudhuria maonyesho ya ndege za kivita mjini Moscow.

Ndege hiyo inalinganishwa na ile ya kivita ya Marekani chapa F-35. 

Marekani ambayo pia ni mwanachama wa NATO imeamua hivi karibuni kuitoa Uturuki katika mradi wake wa ndege ya kivita chapa F-35, baada ya Uturuki kununua kutoka Urusi mtambo wa kinga ya angani dhidi ya makombora, S-400.


from MPEKUZI

Comments