Rais Magufuli Ahutubia Mkutano Wa Sita Wa Jukwaa La Uongozi Afrika Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wastaafu katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Taasisi ya Uongozi baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Somalia Mhe. Hassan Mohamed alipowasili kuhutubia Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019. Wanaofuatia kulia kwake ni Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki na Mfanyabiashara mashuhuri wa Tanzania Bw. Ally Mufuruki

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.


from MPEKUZI

Comments