Lori la mafuta laanguka Kagera....Watu 8 Watiwa Mbaroni Wakiiba Mafuta

Wakati bado Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya  Watu 102 kufuatia ajali ya moto Morogoro ya lori la mafuta, baadhi ya Wananchi wa Kagera wamejitokeza kwa wingi kuchukua mafuta kwenye ajali ya Lori la mafuta lililoanguka jana eneo la Benako Ngara Mkoani Kagera.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewakamata  watu 8 wilayani Ngara, kwa tuhuma  za wizi wa mafuta katika gari  hilo lililopata ajali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera  Revocatus Malimi, amesema pia wamekamata Lita 300 za mafuta, zilizoibiwa kwenye ajali hiyo.


from MPEKUZI

Comments