Jiji La Dodoma Latia Saini Katika Utekelezaji Wa Miradi Mikubwa Ya Maendeleo Ikiwa Ni Pamoja Na Mradi Wa Dodoma City Hotel
Jiji la Dodoma kwa siku ya leo Agosti 27,2019 limevunja Historia baada ya Kusaini miradi Mikubwa ya Maendeleo itakayokuwa inaratibiwa na jiji hilo.
Akizungumza katika utiaji saini wa Miradi hiyo,Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema Jumla ya Miradi itakayotekelezwa ni Saba yenye thamani zaidi ya Tsh.Bil.60 lakini kwa sasa wataanza na miradi miwili yenye thamani ya zaidi ya Tsh.Bil.27.
Kunambi ameitaja miradi miwili ya kuanzia kwa awamu ya kwanza ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Dodoma City Hotel utakaogharimu Bilioni 9.9 lenye ghorofa 11 na Mradi wa pili ni jengo la Uwekezaji litakalokuwa mji wa Kiserikali litakalogharimu zaidi ya Tsh.Bilioni 18.
Aidha,Kunambi amebainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo,unapaswa kutekelezwa ndani ya Mwaka mmoja kuanzia sasa na Miongoni wa Wabia wa Maendeleo watakaochukua tenda hiyo kuwa ni pamoja na Mohammad Builders LTD na Stecol Corporation huku akiwaasa Wadau wengine wa Maendeleo kuchangamkia Fursa hizo.
Katibu tawala mkoa wa Dodoma Kessy Maduka amesema miradi hiyo ni ujenzi wa uchumi wa viwanda wa jiji la Dodoma na linatakiwa liangaliwe katika uwekezaji huku mkuu wa mkoa huo,Dkt.Binilith Mahenge akibainisha kuwa uwekezaji huo unazidi kumuunga Mkono Rais Dokt.John Pombe Magufuli azma ya Makao Makuu na akitoa ombi kwa serikali uboreshaji wa ujenzi wa Shule za Kimataifa.
Kwa Upande wake Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo amesema lengo la Mradi huo ni kutoa unyafuzi wa Mapato ambapo jiji la Dodoma kwa Sasa lina uwezo wa kuwalipa watumishi wake bila utegemezi wa mfuko kutoka hazina kuu huku akibainisha kuwa ujenzi wa majengo hayo ya kisasa itakuwa ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara.
Aidha,Waziri Jafo amewakumbusha watumishi wa Serikali kufanya Kazi kwa Bidii na kuacha maigizo katika utendaji wa kazi.
“Badala ya kufanya kazi watumishi wanajiposti kwenye mitandao ya kijamii wakitaka sifa,hatutaki watendaji wa namna hii”amesema.
Hata hivyo ,Waziri Jafo ametahadharisha kwa wakandarasi wazembe na wababaishaji na hawana nafasi katika serikali ya awamu ya tano.
Katika hatua nyingine,Waziri Jafo amesikitishwa kutokana na wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kushindwa kutekeleza agizo lake ambapo hivi karibuni alitoa agizo kuwa Wilaya hiyo ilitakiwa iwe imeshakamilisha upimaji wa Maeneo hadi kufikia Julai 30,2019 lakini mpaka sasa maeneo yaliyo mengi hayajapimwa na fedha za upimaji serikali ilishatoa.
“Chamwino mnamwaibisha mkuu wa Wilaya,nilitoa maagizo kufikia Mwezi Julai,30,2019 maeneo yote yapimwe wapewe wawekezaji lakini mpaka leo bado.Mnamwaibisha mkuu wetu wa Wilaya ,tena ni eneo la Ikulu sifurahishwi na kitendo hiki.Kwa hiyo nikuagize Dc wa Chamwino uende ukawasimamie wataalam wako na uwachukulie hatua.Maana hakuna kisingizio chochote na Fedha za Upimaji tulishatoa sisi kama serikali.”Amesema Waziri Jafo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia , kazi, vijana ajira,Mhe.Anthony Mavunde amesema katika kutekeleza adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya uwekezaji,mkoa wa Dodoma umeanza utalii wa Mashamba ya Mizabibu.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment