BASATA Wafunguka kuhusu serikali ya Kenya kuufungia wimbo wa 'Tetema' wa Rayvanny na Diamond Platnumz

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limeshangazwa na Serikali ya Kenya kuuzuia wimbo Tetema wa msanii kutoka Tanzania, Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kupigwa kwenye maeneo ya wazi nchini humo.
 
BASATA wamesema wimbo huo ni mzuri kwani hauna tatizo lolote na kawaida yao huwa wanakagua nyimbo zote na kama wimbo ukionekana una matatizo huwa wanachukua hatua ikiwemo kuufungia.

“Tumekuwa tukifuatilia nyimbo za wasanii wa hapa nchini na kuwaita wanapokosea. Tunatoa onyo na hata kufungia nyimbo zao, lakini huu (TETEMA) hauna shida ndio maana nasema sijui wametumia vigezo gani kuuzuia usichezwe mchana,” amesema Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza kwenye mahojiano yake na Gazeti Mwananchi.

Wimbo wa Tetema pamoja na  Wamlabez wa msanii Sailors wa nchini Kenya zimezuiwa kupigwa maeneo ya wazi  nchini Kenya na badala yake zinatakiwa kupigwa katika kumbi za starehe na baa.


from MPEKUZI

Comments