Raia wa Malawi, Paul John (30), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kunajisi mtoto wa miaka saba ili ajiridhishe kingono.
Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hellen alidai Machi 25, mwaka huu eneo la Tegeta Nyuki wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mshtakiwa alimuingiza vidole sehemu za siri mtoto wa miaka 7.
Mshtakiwa alikana kutenda shtaka na Hakimu Mwakalinga alisema dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili Watanzania, wafanyakazi wa taasisi inayotambulika kisheria, barua kutoka kwa waajiri wao na vitambulisho vya kazi.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 10.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment