NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi ccm taifa Kheri James amewataka vijana wenye sifa mkoani Kagera kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali kuanzia serikali za mitaa ili waweze kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.
Bwana Kheri James ametoa kauli hiyo july 27 mwaka huu katika uzinduzi wa Kagera ya kijani uliofanyika katika uwanja wa Hamgembe uliopo katika manispaa ya Bukoba mkoani hapa.
Mwenyekiti huyo amesema vijana ni nguzo kubwa katika ujenzi wa taifa hivyo wajitokeze ili kuwatumikia wananchi wao .
Ameongeza kuwa muda wa kukaa vijiweni kwa vijana umeisha ambapo ametumia muda huo kuwahimiza viongozi waliopitia siasa kuwafundisha vijana wanaowania nafasi mbali mbali katika chama hicho kuwa na maadili mema ndani na nje ya chama hicho.
Ameongeza kuwa vijana watumie fulsa mbali mbali zitakazo wawezesha kupata mikopo kwani serikali ipo bega kwa bega na makundi muhimu likiwemo la vijana katika uzinduzi huo
Bwana James amechangisha shilingi milioni kumi zitakazotumika kuboresha jengo la mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti huku akipongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa katika maendeleo ya Kagera.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment