Uanzishwaji Wa Madawati Ya Jinsia Katika Vituo Vya Polisi Wasaidia Kupunguza Matukio Ya Unyanyasaji Na Ukatili Wa Kijinsia

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh:Samia Suluhu amesema,uanzishwaji wa madawati  Ya jinsia  katika vituo vya polisi vimesaidia kupunguza matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kutoka  watu zaidi ya elfu 96 kwa mwaka 2015 hadi kufikia watu 41 elfu kwa mwaka 2017. 

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya masoko jijini Dodoma,  Mh:Samia  amesema, hadi kufikia mwaka 2017 zaidi ya watu 41 elfu wamepatiwa huduma katika madawati ya jinsia  huku serikali  ikiendelea na mikakati mbalimbali ya kupambana na ukatili huo . 

Hata hivyo amewataka madiwani kutoa fedha kwa vikundi vya wanawake ili kuwezesha uchumi wa vikundi hivyo kuimarika kwa ujumla. 

Awali akimkaribisha makamu wa Rais katika uzinduzi huo Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh:Ummy Mwalimu amesema kuwa kiasi cha laki 5 kinachotolewa kwa vikundi vya akina mama bado havikidhi haja. 

Akitoa salamu za mkoa katika uzinduzi huo Mkuu wa mkoa wa Dodoma dk.Binilith mahenge amesema kuwa kwa sasa hakuna shida dawa katika hospitali kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kutengwa na serikali kutoka million mia tisa hadi kufikia bilioni 4. 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya shinyanga Mh Gulamhafeez Mukadam ambaye ni pia Mwenyekiti wa  Jumuiya ya serikali za Tawala za mitaa na Tawala za mikoa ALAT amesema pamoja na fursa zilizopo katika maeneo ya halmashauri bado kuna changamoto ya kujenga ufahamu,uelewa mwelekeo na dira juu ya dhana nzima ya kutomeza vitendo vya  unyanyasaji  wa  kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya wazi hasa kwa upande wa masoko.

Katika  uzinduzi wa mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya wananwake na watoto katika maeneo ya masoko umeenda sambamba na  zoezi la kukabidhi pikipiki 29 kwa maafisa maendeleo ya jamii ili kurahisisha utendaji kazi wakati wa kushughulikia vitendo hivyo.


from MPEKUZI

Comments