TOUFIQ: Tanzania Kinara Katika Udahili Wa Wanafunzi Elimu Ya Awali Barani Afrika.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).  

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu. 

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni. 

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali. 

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu. 

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.


from MPEKUZI

Comments