Rwakatale Akanusha Habari Za Kujiunga Na Chama Cha Wananchi CUF

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI, KAGERA.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mh wilfredy Muganyizi Rwakatale ametolea ufafanuzi  juu ya uvumi wa kujiunga na chama cha wananchi CUF ambao ulikuwa unasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii siku za nyuma.
 
Akitolea ufafanuzi huo mbunge Rwakatale amesema kuwa alikwenda kwenye ofisi za CUF zilizopo Buguruni Dar es salaam kwa lengo la kuwasalimia baadhi ya viongozi wa chama icho aKiwemo  mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Haruna Lipumba.
 
Mh Rwakatale ameongeza kuwa aliwai kuwa kiongozi wa chama icho kama Naibu katibu mkuu wa chama na wakati anaondoka aliondoka pasipo kuwa na chuki na mtu yoyote ndani ya chama na ndiyo maana wakati anakwenda kuwasabai alipokelewa kwa shangwe.
 
Amewataka watu wanaozusha uvumi huo kuacha tabia hiyo mara moja na kuwataka kumfuata mlengwa ili aweze kutolea ufafanuzi wa jambo husika na kuacha tabia za kuvujisha taharifa za kupotosha umma wa watanzania na kuongeza kuwa ata siku za nyuma aliwai kuzushiwa taharifa za kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM na kudai kwamba haiwezi kutokea ata siku moja kwa kuwa yeye ni mbunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
 
Sanjali na hayo mh Rwakatale amewataka wananchi wa Jimbo la Bukoba mjini kuwaunga mkono katika jitihada za maendeleo kwakipindi hiki ambapo miradi mbalimbali za maendeleo zinaendelea kutekelezwa likiwemo suala la miundombinu za barabara, afya, shule, ukarabati wa meli mpya, michezo , pamoja na ujenzi wa stendi kuu mpya ya mabasi ambayo inajengwa katika kata ya Kyakailabwa mkoani Kagera.


from MPEKUZI

Comments