Raia wa Hungary Akos Berger (28), amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 250 aina ya Amphetamine.
Berger amefikishwa mahakamani hapo Juali 25,2019 na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Maira Kasonde.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai, Julai 19 mwaka huu, eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Kasonde alimtaka mshitakiwa kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa za kulevya, isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP
Upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilka na kesi iliahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu itakapotajwa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment