Iran Yasema inania ya kuanzisha shughuli katika kinu cha nyuklia cha Arak.

Mkuu wa shirika la nishati ya Atomiki la Iran Ali Akbar Salehi amewaambia wabunge wa taifa hilo kwamba nchi hiyo, itaanzisha tena shughuli zake katika kinu cha nyuklia cha Arak. 

Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la habari la ISNA nchini humo. Shirika hilo lilimnukuu mbunge aliyekuwepo katika mkutano huo. Maji mazito yanaweza kutumika katika kinu hicho kuzalisha kemikali ya Pluto-nium inayotumika kutengeneza silaha za nyuklia. 

Mwezi Mei Iran ilitangaza kukiuka makubaliano ya nyuklia na mataifa makubwa duniani, kufuatia Marekani kujiondoa katika makubaliano hayo na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vipya. 

Mnamo Julai tarehe tatu rais wa Iran Hassan Rouhani alisema Iran itaongeza urutubishaji wa madini yake na kuanza kukifufua tena kinu chake cha nyuklia cha Arak Julai 7, iwapo mataifa yaliyotia saini mkataba wa nyuklia hayatolinda biashara na Iran kama yalivyosema makubaliano hayo.


from MPEKUZI

Comments