Jeshi La Polisi Dodoma Lakamata Wahalifu 10 Wanaojihusisha Na Uhalifu Wa Simu Pamoja Na Wahamiaji Haramu Wanne

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwakamata watu kumi (10) wanaojihusisha  na usajili line za simu kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine na kuzalisha line nyingi kwa kitambulisho kimoja bila ridhaa ya mwenye kitambulisho. 

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema kuwa line hizo  wamekuwa wakiuuza kwa wa halifu  na watu wasio na vitambulisho ambao ni wahalifu.

Aidha muroto ameongeza kuwa wamewakamata wahamiaji  wahamiaji haramu wanne ambao ni raia wa Ethiopia huku akisema raia hao wanne walikamatwa katika eneo la chipolo wilayani mpwapwa wakiwa wanasafirishwa katika basi Namba T.112 ATC SCANIA Bus la Kampuni ya Premere  line linalofanya safari  kutoka mwanza kwenda mbeya.

Hatahivyo, kamanda muroto amesema kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa yote wameanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ambavyo sasa wanasaidia jeshi la polisi kuwaibua wahalifu wote katika mitaa yao wanaohifadhi wahalifu pamoja na wapokeaji wa mali zinazotokana na uhalifu.

Katika hatua nyingine kamanda muroto amewataka Madereva kuheshimu sheria za usalama  barabarani huku akisema kuwa anayetembea kwa miguu ana haki ya kisheria kama dereva anaye endesha barabarani.

Methew Benjamini ni Mrakibu msaidizi,wa jeshi la polisi, Mkuu wa kitengo  cha usalama barabarani  mkoa wa Dodoma  amesema wameamua kujikita katika utoaji wa elimu zaidi  ya usalama  barabarani hasa katika vivuko vya waenda kwa miguu ambapo zaidi ya asilimia 76 ya ajali za barabarani hapa nchini husababishwa na makosa ya kibinadamuikiwa ni pamojana uzembe  wa madereva. 

Nao watembea kwa miguu wamesema kuwa walikuwa hawana elimu ya kutosha juu ya vivuko hivyo vya watembea kwa miguu huku wengine wakitoa ushauri kwa madereva kufuata sheria za barabarani


from MPEKUZI

Comments