Gavana Shilatu Ashangazwa Na Diwani Kutofuatilia Upatikanaji Wa Mikopo Ya Vijana, Wanawake Na Walemavu.

Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amembana Diwani wa Chama Cha Wananchi (CUF) Kata ya Mkoreha Mhe. Ahmad Ally Ndende juu ya utolewaji wa mikopo ya Halmashauri kwa Vijana, Wanawake na Walemavu ili kuwakwamua Wananchi kiuchumi.

Hayo yamejitokeza kwenye mkutano na Wananchi wa Kijiji cha Dinyeke kata ya Mkoreha ambapo Gavana Shilatu aliitisha ili kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinazowakabili.

Gavana Shilatu alimuuliza Diwani huyo kuelezea ni vikundi vingapi mpaka sasa vimenufaika na mikopo nafuu kwa Vijana, Wanawake na Walemavu toka Halmashauri ikiwa yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya kata.

*_"Hakuna wanufaika wa mikopo hiyo ya 10% toka Halmashauri kwani vikundi vingi havijasajiliwa na havina miradi."_*  Alijibu Diwani Ndende.

Gavana Shilatu alisisitiza kazi ya viongozi ni kuonyesha njia ya kuwakwamua Wananchi kiuchumi pasipo kukwepa majukumu wala kuingiza ubaguzi.

Gavana Shilatu alisisitiza kuwa viongozi tunatakiwa kuhamasisha Vijana, wanawake na walemavu kuwatengenezea mazingira ya kuwa na vikundi vyenye katiba vilivyosajiliwa na vyenye shughuli maalumu ili waweze kupata mikopo hiyo.

_"Sisi viongozi tunajukumu la kuwaonyesha njia Wananchi na si kutumia mwanya wa kutokuelewa kwao kama njia ya kuwakosesha *FURSA MUHIMU* kama ya Mikopo nafuu toka Halmashauri. Na mikopo hii inatolewa kwa haki pasipo ubaguzi wa kiitikadi."_  Alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo ulihudhuliwa na Diwani kata ya Mkoreha, Mtendaji Kata ya Mkoreha, Mtendaji Kijiji cha Dinyeke, Serikali ya Kijiji cha Dinyeke pamoja na viongozi wa Vitongoji.


from MPEKUZI

Comments