Bunge Limepitisha Muswada Wa Sheria Ya Marekebisho Ya Sheria Mbalimbali Namba 3 Wa Mwaka 2019 Unaofanyia Marekebisho Sheria 8 Ambazo Ni Sheria Za Makampuni, Hakimiliki, Filamu Na Michezo Ya Kuigiza, Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali, Takwimu, Vyama Vya Kijamii, Uwakala Wa Meli Na Miunganisho Ya Wadhamini.
Akisoma mapendekezo hayo bungeni mwanasheria mkuu wa serikali Prof. Adelardus Kilangi amesema Madhumuni ya marekebisho ya kila sheria ni kuondoa migongano kwa sheria ya makampuni juu ya msajili na msimamizi wa asasi,kuweka namna bora ya usimamizi,kuweka mipaka ya usimamizi ,usimamizi wa asasi pamoja na kuongeza kiwango cha adhabu na kuongeza mapato katika sekta ya Filamu.
Mkatika sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali imeweka wigo wa mashirika yatakayoruhusiwa kusajiliwa kama NGO’s kuwa ni yale yanayolenga kunufaisha jamii na sio wanachama wake.
Katika hatua nyingine,Prof. Kilangi amesema katika sheria ya takwimu muswada huo unapendekeza kuanzisha kamati ya kitaalam itakayokuwa na jukumu la kupokea na kujadili malalamiko yanayotokana na wadau kuhusu usahihi wa takwimu zilizotolewa kwa umma.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge katiba na sheria Najma Giga akiwasilisha maoni ya kamati hiyo amesema Wakati umefika sheria zinazoratibu na kusimamia sekta ya sanaa zioanishwe na masharti ya sheria na ulinzi kwa maendeleo ya wadau husika wa sanaa na Taifa kwa Ujumla.
Aidha, kamati inapendekeza msajili kutoa onyo kwa notisi ya muda wa siku 30 itakayoitaka taasisi husika kurekebisha kasoro au makosa iliyoyafanya kabla ya kuchukua hatua ya kusimamisha shughuli zake.
Katika Mapendekezo ya kamati ilibaini ibara 19 zenye Dosari mbalimbali za kimaandishi ambazo zinahitaji marekebisho na zimekubaliwa na serikali katika marekebisho .
Ibarahizo ni Ibara ya 4,Ibara 6,Ibara ya 10,Ibara ya 16,ibara ya 17,Ibara ya 18,ibara ya 20,ibara ya 25 ,ibara ya 27,ibara ya 35,ibara ya 36,ibara ya 42,ibara ya 47,ibara ya 50,ibara ya 50,ibara ya 52,ibara ya 55,ibara ya 61,ibara ya 62 na Ibara ya 73.
Mapendekezo mengine ya Kamati ya bunge,katiba na sheria ni kuwepo kwa maboresho kwa sheria mahususi kwa Tasnia ya Filamu ,Sanaa,Ubunifu na utalii nchini kwani wasanii wengi wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kutokuwepo kwa sheria madhubuti hivyo serikali ni vyema kukamilisha mchakato wa sheria .
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment