BREAKING: Tundu Lissu Avuliwa Ubunge......Spika Ndugai Ataja Sababu

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameliambia Bunge hilo leo Ijumaa Juni 28, 2019 kuwa amewandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumjulisha kuwa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lisu kipo wazi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge ambapo ametaja mambo mawili yaliyomponza Mnadhimu Mkuu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni kutojaza taarifa za mali na madeni na sababu ya pili kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.

Ndugai amesema hajamfukuza Lissu bali Katiba ndiyo imemuondoa mbunge huyo ambaye kikao chake cha mwisho cha Bunge kilikuwa Septemba 7, 2017 ambapo mchana wa siku hiyo alipigwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake Area D jijini Dodoma.

Mara baada ya kushambuliwa, alipekewa Hospitali ya Rufaa Dodoma kisha usiku huo huo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako alikaa hadi Januari 6 mwaka 2018 alikohamishiwa nchini Ubelgiji aliko mpaka sasa.


from MPEKUZI

Comments