Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Tanzania haina upungufu wa nguzo za umeme, nyaya wala transfoma hivyo akaomba wakandarasi wa umeme kuacha visingizio.
Dk Kalemani ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatatu Mei 27, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Nyang’ hwale (CCM), Hussein Amar.
Mbunge huyo ametaka kujua ni kwa nini mkandarasi wa umeme katika jimbo lake ametandaza nguzo lakini hafungi umeme kwa kisingizio cha upungufu wa nyaya.
Waziri amesema kauli kuwa hakuna nyaya za umeme haina ukweli kwani katika kipindi hiki hakuna upungufu wowote kuhusu vifaa hivyo na akaonya kwa wakandarasi wanaotoa sababu hizo waache mara moja na badala yake wakafunge umeme kwa wakati waliopangiwa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment