Wakala wa usajili ufilisi na Udhamini nchini RITA Watoa wito kwa jamii kuhamasika katika swala la usajili wa vifo

Na Amiri kilagalila-Njombe
Wakala wa usajili ufilisi na Udhamini nchini RITA umetoa wito kwa jamii kuhamasika katika swala la usajili wa vifo kutokana na manufaa mbali mbali yanayotokana na zoezi hilo.

Akizungumza juu ya umuhimu wa faida za usajili wa vifo,kaimu kabidhi wasii mkuu,afisa mtendaji mkuu RITA Bi.Emmy Hudson akiwa mkoani Njombe amesema kuwa ni muhimu vifo vyote kusajiliwa mara vinapotokea ili kupata nyaraka ya kisheria inayothibitisha kutokea kwa kifo kutokana na faida mbali mbali.

“Ni muhimu sana vifo vyote visajiliwe mara tu vinapotokea hata vya watoto walio zaliwa ndani ya dakika chache na kufariki,cheti cha kifo huwasaidia wafiwa kushughulikia maswala ya mirathi ya marehemu kama nyumba ardhi,pamoja na mjane au mgane,watoto kulipwa mafao na pensheni ya marehemu lakini pia kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu ambao wamefiwa na wazazi wao kupata afua ya mkopo”alisema Bi Emmy Hudson

Pamoja na manufaa wanayoyapata wananchi afisa mtendaji mkuu wa Rita amesema,serikali pia inahitaji taarifa na takwimu sahihi za vifo ili kusaidia kupata takwimu sahihi ya idadi ya watu baada ya idadi yake kutolewa katika mfumo wa idadi ya watu walio hai.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mh.Adrea Tsele kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,amewataka watendaji na wadau mbali mbali kushirikiana kwa kasi katika kubadili asilimia 23 ya usajili wa vifo ili kufikia asilimia za kuridhisha.

“Uoga tulionao unasababisha wananchi wengi kuto kusajili matukio haya mara yanapotokea hivyo kama nchi kuwa na wastani wa asilimia 17 ya vifo kitaifa na 23 kwa mkoa wa Njombe takwimu hii sio ya kuridhisha kwa hiyo ni imani yangu kwamba tunaenda kubadili hali hii kama ilivyo kwa usajili wa watoto wadogo tulikuwa asilimia 8.5 na ndani ya miezi mitatu tukaweza kufikia asilimia 100 hivyo naamini tutafanikisha zoezi hili kwa kasi hiyo hiyo”alisema Adrea Tsele

Aidha mkoa wa Njombe umeadhimia kufikisha asilimia 100 ya usajili wa vifo ndani ya miezi mitatu.


from MPEKUZI

Comments