TANESCO Kuanza Kutoa Gawio Serikalini

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa sasa halihitaji ruzuku kutoka serikalini na kuanzia mwaka 2019/20 litaanza kutoa gawio.

Amesema Tanesco  imeanzisha utaratibu mpya wa mawasiliano baina ya wateja na Tanesco kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo kuanzisha makundi ya WhatsApp kwa kila wilaya yanayopatikana saa 24 ili  kuimarisha huduma kwa wateja, kuongeza ufanisi na mapato ya shirika hilo.

Akizungumza  jana Jumanne Mei 28, 2019 akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo alisema Tanesco kwa sasa haihitaji ruzuku ya Serikali katika shughuli zake za uendeshaji kutokana na kujiendesha lenyewe na kuokoa wastani wa Sh143 bilioni zilizokuwa zikitumika kama ruzuku kutoka serikalini kila mwaka.

“Kuimarika kwa mapato ya Tanesco kwa kiwango cha ongezeko la asilimia 1.5 mwaka 2017/18 hadi asilimia 7.6 mwaka 2018/19. Hivyo ni matarajio kuwa Tanesco itaweza kuanza kutoa gawio serikalini katika kipindi cha mwaka 2019/20,” alisema

Alisema imeunganishia umeme wateja wapya 969,431 katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Mei 15, 2019 na kufikia wateja 2,442,648 ikilinganishwa na wateja 1,473,217 waliokuwepo kuanzia nchi ilipopata uhuru hadi Juni, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 66 kwa miaka mitatu.


from MPEKUZI

Comments