Serikali Yaanza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Mpango Miji Ambapo Maeneo Yaliyoiva Kuwa Miji Yafikia 455 Hapa Nchini.
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali imeanza utelekelezaji wa mkakati wa kupanga miji yote nchini ambapo maeneo yaliyofikia kuwa miji hadi sasa ni Zaidi ya 455.
Serikali imeanza utelekelezaji wa mkakati wa kupanga miji yote nchini ambapo maeneo yaliyofikia kuwa miji hadi sasa ni Zaidi ya 455.
Hayo yamesemwa leo Mei 29,2019 na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kasulu mjini Daniel Nicodemus Nsanzugwako aliyehoji kwanini serikali isije na mkakati endelevu wa kupanga miji yote iliyotangazwa kwenye gazeti la serikali.
Katika majibu yake,Waziri Lukuvi amesema serikali imeanza utekelezaji wa mkakati wa kupanga miji yote ambayo imetangazwa kwenye gazeti la Serikali kwa kuandaa mipango kabambe ya majiji,manispaa,na miji.
Aidha,Serikali imeainisha maeneo yote ambayo yameiva kuendelezwa kimji kwa ajili ya kuyatangaza kwenye gazeti la serikali kuwa maeneo mipango ambayo ni Zaidi ya maeneo 455 nchini.
Hata hivyo,Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa kifungu Na.7[1] na 5 cha Sheria ya Mipango miji Na.8 ya mwaka 2007,jukumu la kupanga na kupima miji ni la mamlaka za upangaji ambazo ni Halmashauri za majiji,manispaa,miji ,na mamlaka za miji midogo.
Waziri Lukuvi amebainisha,Serikali imeendelea kuzisaidia halmashauri kupanga na kupima miji yao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo mwaka 2018/2019 serikali kupitia Wizara imetoa Jumla ya Shilingi Bilioni 6.4 kwa halmashauri 29 nchini kwa ajili ya upangaji,upimaji na umilikishaji wa ardhi .
Pia imewezesha uandaaji wa mipango kabambe ya miji 18 kupitia program ya kuzijengea uwezo mamlaka za miji [Urban Government Strengthening Program-ULGSP] Chini ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment