Olesendeka aridhishwa na ukamilishwaji wa kituo kipya cha mabasi Njombe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amefanya ukaguzi katika kituo kituo kipya cha mabasi kitakachogharimu zaidi ya bil 9.6 Hadi Kukamilika Kwake pamoja na ujenzi wa mradi wa soko kuu mjini Njombe lenye hadhi ya kimataifa litalogharimu bil 9.3 na kuonyesha kuridhishwa na mwenendo wa ukamilishaji wa miradi hiyo inayofadhiliwa na benk ya dunia.

Pamoja na kuridhishwa na ujenzi unaoendelea akiwa katika kituo cha mabasi ambacho kilianza kufanya kazi Mei  11 kwa agizo la rais ,mkuu wa mkoa amepokea malalamiko kutoka kwa abiria,machinga,mama na baba lishe ambao wanasema wanashindwa kufanya biashara kama ilivyokuwa awali katika stendi ya zamani kwani halmashauri imezuia kufanya biashara ndani ya stendi hata kwa wenye vitambulisho vya mjasiriamali.

"Unapotoka toka pale ile lisiti waliyonipa wanachana natoka tena kuchukua abiria ninavyoingia nalipa tena mia mbili sasa kuanzia saa kumi na mbili ile asubuhi mpaka saa moja jioni ninakuwa nimelipa shilingi ngapi,lakini humu ndani hakuna mboga wala cha nini kuna mwingine anahitaji mboga mfano samaki aende nazo kijijini hamna haya chungwa hamna" walisema baadhi ya wajasiriamali ndani yastendi

Mara baada ya kusikiliza kero hizo Christopher Olesendeka anawataka Wajasiliamali Hao Kuvuta Subira Wakati Yakiwekwa Sawa Mazingira Ya Wao Kufanya Biashara Ndani ya Stendi Hiyo Baada ya Ujenzi Wake Kukamilika.

"Nataka niwahakikishieni mheshimiwa Rais ametoa fedha kwa ajili ya stendi hii na akaelekeza kituo hiki cha mabasi kikamilike haraka ili ninyi kina baba lishe na mama lishe muweze kufanya biashara katika maeneo mazuri zaidi,tunaendelea kukagua kuonamaeneo yaliyobaki ili stendi ikamilike vizuri halafu tuendelee kuungana na halmashauri yenu tuweke utaratibu rafiki ili kuona wanyonge wa Njombe ndio watakaonufaika na vibanda vilivyoko stendi na uendeshaji wabiashara katika eneo hili''

Katika hatua nyingine Olesendeka amekagua ujenzi wa soko kuu ambao Ameonyesha kuridhishwa na kasi na ubora katika ujenzi Huo  huku Mhandisi wa mradi huo Mboka Justin akidai mradi umefika asilimia 60 na kuahidi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.


from MPEKUZI

Comments