Upelelezi wa Kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride inayomkabili mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45) bado haujakamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka amedai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauonba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.
Wakili Wankyo ameeleza kuwa amesikia kilichozunguzwa na upande wa utetezi, hivyo watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.
Hakimu Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi June 10, 2019, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment