Serikali Yaikatalia Kenya kujenga mabwawa ya uzalishaji umeme katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Serikali imeikatalia Kenya kujenga mabwawa ya uzalishaji umeme katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hayo yamesemwa leo Aprili 29, Bungeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Amina Molel (CCM), ambaye alitaka kujua Tanzania inachukua hatua gani kuhusu suala hilo.

Katika swali lake Amina amesema kuna taarifa kwamba nchi ya Kenya inatarajia kutekeleza mpango wa kujenga mabwawa makubwa kwa ajili ya uzalishaji umeme ambao unatishia ustawi wa uwepo wa hifadhi ya Serengeti.

Akitoa majibu ya swali hilo Kanyasu amesema uchunguzi ulibaini utekelezaji wa miradi hiyo ungesababisha athari kubwa kwa ikolojia ya hifadhi hiyo na utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka Kenya kuhalalisha miradi hiyo hazikuwa sahihi.

Aidha Kanyasu amesema miongoni mwa athari hizo ni pamoja na kuhatarisha ustawi na maisha ya viumbe hai kutokana na ukosefu wa maji katika Mto Mara wakati wa Kiangazi.


from MPEKUZI

Comments