Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM), amesema elimu ya Tanzania ni kama kifungo cha maisha.
Akichangia mjadala wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, bungeni leo Aprili 30, Kishimba amesema muda wa kusoma shule Tanzania ni mrefu na unachangia vijana kuzeeka kabla ya kuanza kufanya kazi.
Amesema ni vyema mwaka mmoja mwanafunzi asome madarasa matatu ili kuokoa muda wa kuchukua miaka mingi kabla ya kumaliza shule.
Kishimba ameishauri Serikali iunde tume ya kukusanya maoni kuhusu elimu kwa sababu hali ni mbaya, kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu lakini wapo mtaani kila kona na hawana faida yoyote.
“ Nashauri serikali iunde tume wananchi watoe maoni ni elimu ipi tuwe nayo.
“ Hivi ni utafiti gani unaosema ubongo wa binadamu kila mwaka usome darasa moja”? tufanye mabadiliko makubwa kwenye sera hii, wenzetu Afrika Kusini nao wanateseka na mfumo kama huu,” amesema Kishimba.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment