Kundi kubwa la wanayama aina ya fisi limewajeruhi watu watano sehemu mbalimbali za miili yao katika kata za Nyandekwa na Kilago halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wakati wakijaribu kupambana na fisi hao waliovamia makazi ya watu.
Diwani wa Kata ya Kilago PETER EMANUEL amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia April 28,2019 ambapo majeruhi watatu hali zao bado hazijaimarika na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mji wa Kahama na kwamba wananchi katika maeneo hayo amejawa na hali ya wasiwasi.
Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama, baadhi ya majeruhi wameiomba serikali kuwadhibiti fisi hao kwani wanaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi na kwamba wamekuwa wakipambana nao mara kwa mara.
Afisa maliasiri halmashauri ya mji wa Kahama, THOMAS MANUMBU amesema tatizo la Fisi kuvamia makazi ya watu bado lipo kwa wingi katika kata za pembezoni tangu mwezi wa pili mwaka huu huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati serikali inaendelea kupambana na fisi hao.
Kwa upande wake Mhifadhi wa wanyanama Tanzania (TAWA) wilaya ya Kahama, MAPANYA KARUTO amewataka wananchi kutumia toshi nyakati za usiku na kwamba waondokane na imani za kishirikina dhidi ya uwepo wa fisi hao.
Credit;kahama Fm
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment