Wakenya wazuia magari ya Tanzania kuingia kwao, wafanya fujo na kuchoma matairi

Wakazi wa mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga upande wa Kenya wamezuia magari kutoka Tanzania kuingia nchini mwao, kwa madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu wa kubadili fedha za kigeni wa nchini mwao hapo jana Jumanne, Machi 26 majira ya saa 3 usiku

Mmoja wa wananchi waliokuwa katika eneo hilo, Odinga Nguduu amesema kuwa, majira ya saa tatu ilikuja gari yenye namba za Tanzania kwenye Ofisi ya mfanyabiashara huyo na aliondoka naye kuelekea Namanga upande wa Tanzania.

"Tangu achukuliwe jana usiku hajarudishwa na hadi sasa haonekani mtu wetu, wakimrejesha tutaacha vurugu na tutaruhusu magari haya ya abiria na mizigo kuingia Kenya" amesema
 
Naye Simon Ledupa Mkazi wa Namanga ya Tanzania amesema kuwa Namanga ni mpaka mkubwa na kuna watu wengi kutoka mataifa mbali mbali wanapita hapa, mtu huyu wanayedai ametekwa na Watanzania si kweli yupo humo humo kwao.


from MPEKUZI

Comments