Serikali Yaweka Mapingamizi Matatu Kesi Ya Joshua Nassari Kupinga Kuvuliwa Ubunge

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imepanga March 29, 2019 mwaka huu kutoa uamuzi wa mapingamizi matatu yaliyowekwa na upande wa Serikali hii leo katika kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi kwa ajili ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge wa kumfutia ubunge Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Utakumbuka, Machi 20 mwaka 2019 mahakama ilitoa siku 7 kwa upande wa Serikali kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo.Jaji aliagiza pia kusifanyike uchaguzi wowote jimboni hadi hapo maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.


from MPEKUZI

Comments